Tetesi za Soka barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Manchester City itapaswa kuongeza juhudi kumpa mkataba wa muda mrefu winga wa England Raheem Sterling, 26 ambaye anahusishwa na Barcelona, ili aweze kusalia klabuni hapo.

Manchester United imeungana na vilabu vingine, vikiwemo Tottenham na Newcastle United, kutaka saini ya mshambuliaji Mserbia Dusan Vlahovic, 21 kutoka Fiorentina.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Zinedine Zidane wakijiweka sawa na uwezekano wa kocha wao Mauricio Pochettino kuondoka na kujiunga na Manchester United.

 

Zidane Akataa Kazi Manchester United.

Ralf Rangnick anatarajiwa kuwa kocha wa muda wa Manchester United lakini awali alikataa ofa kutoka klabu hiyo ya Old Trafford kabla ya kukubali masharti mapya ya mkataba huo.

Tetesi zinasema, Manchester United bado inamsaka Pochettino kuchukua mikoba ya umeneja msimu unaokuja, licha ya kuwasili kwa Rangnick.

Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 26, anawaniwa na Manchester United kama mbadala wa Paul Pogba, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford unakwenda kumaliza mwishoni mwa msimu.

Barcelona wanafikiria kutupa ndoano kumsajili mshambuliaji wa Basel, Arthur Cabral lakini itabidi wauze baadhi ya wachezaji kabla ya kuu kupeleka ofa kwa mbrazil huyo mwenye miaka 23.

 

Inter Milan wanamatumaini kwamba kiungo wake Mcroatia Marcelo Brozovic,29 atasaini mkataba mpya, mkataba wske wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Kocha wa AC Milan Stefano Pioli, 56, siku ya leo atasaini mkataba mpya kuongeza miaka miwili zaidi na kusalia katika klabu hiyo ya Serie A.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.