Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amethibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Klabu hiyo ya Uhispania alitoa taarifa fupi iliyotangaza kwamba kocha huyo wa miaka 48 amepata maambukizi ya virusi vya corona lakini haikutoa taarifa zaidi kuhusu hali yake au ikiwa hilo litaathiri kwa namna yoyote ile kikosi chake.


Zidane anapitia shinikizo kwa matokeo mabaya ya timu hiyo ya Real ikiwemo mechi ya Jumatano katika taji la Copa del Rey waliposhindwa na timu ya Alcoyano.

Real Madrid, ikiwa ni ya pili baada ya mahasimu wao Atletico katika Ligi ya La Liga itachuana na Alaves Jumamosi .

Kupoteza mchezo dhidi ya Alcoyano kunawadia ikiwa ni wiki moja baada ya kuondolewa kwenye kombe la Super Cup na Athletic Bilbao.

Real Madrid inayoshika nafasi ya pili katika jedwali imecheza mechi 18, wakiwa alama 7 nyuma ya Atletico, ambayo ina mechi 2 ambazo haijacheza.


USHINDI UPI NI MKUBWA KWAKO, £2,000,000? 🤑

Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.

INGIA MCHEZONI


12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa