Kocha wa timu ya Westham United David Moyes amesema kuwa mwamuzi aliyekuwa akichezesha mechi kati yao na Chelsea aliamua vibaya uamuzi wa kulikataa goli la kusawazisha ambalo walifunga katika kipindi cha pili.

Moyes amesema kuwa goli hilo hakuona kama mchezaji wake alimchezea madhambi golikipa wa Chelsea Mendy, hivyo maamuzi ya refa kulikataa goli hilo ni kuwa amekosea ambapo mechi hiyo ilimalizika kwa Westham kupoteza kwa mabao 2-1.
Westham ambayo jana walikuwa ugenini wamekuwa hawana matokeo mazuri toka walipoanza ukilinganisha na msimu uliopita kwani walikuwa wapo imara zaidi na walileta ushindani ndani ya ligi lakini mpaka sasa wamekuwa wa baridi sana.

Moyes na vijana wake ndani ya michezo sita wameshinda mmoja, sare moja na wamepoteza michezo minne kitu ambacho sio kawaida kwa wagonga nyundo hao wa London. Sasa wanapoteza mechi kila kukicha wakijitahidi wanapata sare.

