Mwakinyo: "Nimeumia kupoteza Pambano, Hujuma zimechangia"

The Champion Boy, Hassan Mwakinyo katika hali ambayo imewaacha wengi na maswali ni namna ambavyo pambano lake la usiku wa leo Septemba 4 kupoteza kwa Technical KnockOut “TKO”, dhidi ya Liam Smith katika raundi ya 4.

Mwakinyo: "Nimeumia kupoteza Pambano, Hujuma zimechangia"

Mara baada ya pambano hilo, Mwakinyo aliweza kuzungumzia jinsi ilivyokuwa kabla ya yeye kupanda ulingoni ambapo kwa ufupi amesema, hujuma ni chanzo cha yeye kupoteza pambano hilo.

“Hujuma ambayo ilitokea kabla ya mechi, begi langu la vifaa lilipotelea kwenye uwanja wa ndege “Amsterdam” kwa siku3, leo wamenipa vifaa vyao vya kupigania “viatu’ kitu ambacho kilisababisha nijihisi kuwa na mechi”

“Najua nimewaumiza mashabiki zangu, hata mimi nimeumia hakuna anayependa kupoteza pambano, ila promota kaniambia mechi itarudiwa.” Alisema Mwakinyo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Salim Kikeke ️ (@salim_kikeke)

Rekodi za Hasaan Mwakinyo.

Mwakinyo alianza safari yake ya kupigana mwaka 2015 huko Jijini Tanga.
Mwaka 2016 alipambana na Shabani Kaoneka na kupigwa kwa KO lakini hakuishia hapo aliendelea kupambana mpaka hii leo.

  • Ushindi wa KO dhidi ya Mnabia Anthony Jarmani kule nchini Botswana ulimpatia rekodi ya Kimataifa, ambapo alipata mkanda wa WBA “Pan African super-welterweight” mwaka 2017.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Dr. Fredrick Bundala (@skytanzania)

  • Alipambana na Mrusi Lendrush Akopian na kupigwa katika raundi ya 4.
  • Mwakinyo alishinda taji la Shirikisho la Ngumi Duniani la Mabara (The World Boxing Federation Intercontinental title) mwaka 2020 na kufanikiwa kulitetea mara moja ikiwa ni katika mapambano yake matatu ya mwisho.

Mwakinyo: "Nimeumia kupoteza Pambano, Hujuma zimechangia"

  • Moja ya rekodi kubwa kuwahi kuiweka ni ile ya kumkalisha bingwa wa zamani wa dunia Julius Indongo mnamo Septemba 2021, na kuimarisha sifa za Mwakinyo zilizowekwa kwa heshima ya ushindi wake dhidi ya Eggington.

Rekodi yake ya sasa AMESHINDA jumla ya mapambano 20 (14 kwa KO) na kupoteza mara tatu ukijumlisha na hilo la jana 3 Septemba 2022.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.