Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema kuwa haimtambui mchezaji ambaye amesajiliwa na klabu ya Young Africa Tuisila Kisinda msimu huu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

TFF imesema kuwa Kisinda hatakuwa kati ya wale wachezaji wa kigeni 12 ambao watacheza msimu huu kutokana na Yanga kuchelewesha usajili wa winga huyo ambae walimsajili kutoka RS Berkane ambapo alienda msimu uliopita klabuni huko ambayo ipo nchini Morroco.
Sakata hilo la Kisinda kutotambulika na TFF limeleta sintofahamu kwa baadhi wa wadau na wapenzi wa mpira hap[a Tanzania ambapo sheria zinasema kuwa ili mchezaji aweze kucheza inabidi akamilishe vitu vyote vinvyohitajika na awe na Leseni, Lakini ili mchezaji huyo aweze kucheza michuano ya klabu bingwa na shirikisho Africa mchezaji huyo lazima awe na leseni ya CAF.

Na kwa upande wa Yanga majina ya wachezaji 12 wa kigeni yalishawasilishwa CAF, hivyo Yanga kuomba kuwa jina la Kambole litolewe liingizwe la Kisinda ili aweze kucheza lakini kutokana na kanuni na sheria za CAF mchezaji ili atolewe jina lake inabidi asajiliwe kunako klabu nyingine ndipo jina lake litolewe sio tu litolewe kisa jina lingine linataka kupachikwa. Na ndio maana TFF inasema mchezaji huyo hawamjui.

