Baada ya ligi kuu Tanzania bara kuisha NBC Premier League sasa ni muda wa mdhamini wa ligi hiyo kutoa zawadi kwa washindi wote wa ligi na wachezaji waliofanya vizuri kwenye msimu uliosha na tuzo za mwaka huu zimepewa jina la NBC TFF AWARDS 2022.

Sherehe za ugawaji wa tuzo za NBC TFF AWARDS 2022, zitafanyika kwenye ukumbi wa Rotana Hotel jijini Dar es salaam, huku mdhamni mkuu akiahidi sherehe za ugawaji tuzo kwa mwaka huu zitakuwa kubwa na zatofauti.

NBC TFF AWARDS 2022

Jumla ya tuzo binafsi 57 kutolewa, huku tuzo za zaidi ya mtu moja mazo zitatolewa kwa Seti Bora ya Waamuzi, Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya Wanawake na Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya NBC.

Sherehe za ugawaji  tuzo  za NBC TFF AWARDS 2022 zinatarajiwa kuanza saa kumi na mbili jioni, pia usiku huo mshindi wa kwanza, pili, tatu na nne nao watapatiwa zawadi zao kwenye sherehe hizo.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa