Klabu ya Wolveshampton Wonderers inatarajia kumsajili Diego Costa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea na Atletico anayecheza kama mshambuliaji. Mchezaji huyo anatarajiwa kuwa Uingereza wiki hii kwaajili ya kukamilisha uhamisho wake akitokea Atletico Mineiro ya huko Brazil. Diego anasajiliwa na Wolves akiwa kama mchezaji huru ambapo mkataba wake utakuwa hadi June 2023

Inaripotiwa kuwa Wolves wapo kwenye mazungumzo ya kina kwaajili ya kumsajili mshambuliaji huyo huku kukiwa na makubaliano katika kanuni juu ya makataba wa mchezaji huyo. Mpango huo unategemeana na vipimo vya matibabu ambavyo tayari vimepangwa na klabu hiyo.
Diego Costa mwenye umri wa miaka 34 amepita vilabu mbalimbali ikiwemo Chelsea ya Uingereza ambapo alicheza kwa mafanikio makubwa, Atletico Madrid ya Hispania Valladolid na vilabu vingine vingi kabla hajatimkia huko Brazil.

Wolves ambayo inaongozwa na kocha mkuu Bruno Lage hawajaanza msimu vizuri kwani ndani ya michezo sita ambayo amecheza ameshinda mchezo mmoja, sare tatu na amepoteza michezo miwili huku akiwa anashikilia nafasi ya 14 kwenye msimamo. Diego Costa atakuja kuongeza faida kwenye eneo la ushambuliaji kwani ni mchezaji mzoefu na anaijua ligi ya Uingereza.

