Wolves Kumpa Neves Mkataba Mpya

Klabu ya Wolveshampton WonderersΒ  inatarajia kumpatia mkataba mpya mchezaji wake Ruben Neves mwenye umri wa miaka 25 na ambaye anacheza katika eneo la kiungo mkabaji, ambapo kocha mkuu wa timu hiyo Bruno Lage akithibitisha hilo.

 

Wolves Kumpatia Neves Mkataba Mpya

Kocha huyo aliendelea kwa kusema kuwa wanahitaji muda kwaajili ya kupanga mkataba wa mchezaji huyo. Vilevile amesema kuwa wakati wa siku ya mwisho ya kufungwa dirisha la usajili klabu ya Liverpool hawakuwakaria Wolves kwaajili ya kumsajili kiungo huyo bali walimhitaji kwa mkopo.

Liverpool ilikuwa ikihitaji kiungo baada ya wachezaji wake wa eneo la kiungo na ulinzi kupata majeraha hivyo wakamtaka kwa mkopo lakini haikuwezakana na baadae wakahamia kwa kumsajili Arthur Melo kutoka Juventus.

Wolves Kumpatia Neves Mkataba Mpya

Wolves mpaka sasa pale ligi kuu ya Uingereza yupo nafasi ya 18 chini kabisa huku akiwa amecheza mechi tano hajashinda mchezo wowote, sare tatu na kupoteza michezo miwili, Na leo atakuwa nyumbani akimkaribisha Southampton.

Acha ujumbe