Lionel Messi MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Argentina anayekipiga katika klabu ya Paris-Saint-Germany (PSG), ni moja ya Nyota wenye mafanikio zaidi kwenye ulimwengu wa soka.

Rekodi za Messi ni nyingi sana ambazo chache kati ya hizo ni ile ya kuwa mchezaji namba moja mwenye Ballon d’Or nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote yule akiwa na tuzo hizo mara 7 akifuatiwa na mshambuliaji wa Ureno anayekipiga kwenye Klabu ya Man Utd Cristiano Ronaldo ambaye ameshinda mara tano “5”.

Katika orodha ya wachezaji wanaowania Ballon d’Or ambayo itatolewa mwaka Oktoba 2022, Messi hajajumuishwa kwenye orodha hiyo ambayo ina washambuliaji kama Robert Lewandowski wa Barcelona, Cristiano Ronaldo wa Man utd, Karim Benzema wa Real Madrid na Mohammed Salah wa Liverpool.

Zifuatazo ni takwimu za msimamo wa ballon d’or kwa Lionel Messi.
- Mwaka 2006 ilikuwa ni mara ya kwanza kwa nyota huyo kushiriki na aliishia nafasi ya 21.
- Mwaka uliofuata 2007 akashika nafasi ya 3.
- Mwaka 2008 alishika nafasi 2.

- Kuanzia mwaka 2009 mpaka mwaka 2012 alichukua Ballon d’OR mfululizo mara 4.
- Mwaka 2013-2014 aliishiua kuwa nafasi ya 2

- Mwaka uliofuata 2015 akachukua tenaikiwa ni Ballon d’or yake ya 5.
- Mwaka 2016, 2017, 2018 hakuchukua aliishia nafasi ya 2 kwa miaka miwili huku mwaka wa 2018 haukuwa mzuri sana kwake kwani alishuka mpaka nafasi ya 5.
- Mwaka 2019 na mwaka 2021 alichukua na kumfanya achukue mara 7

Mwaka 2020, Tuzo hizo hazikuweza kufanyika kutokana na wimbi la ugonjwa wa Uviko 19.

