Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameahidi kumrudisha aliyekuwa mchezaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi kwenye viunga vya Camp Nuo kwa mara pili baada ya kuondoka kwenye klabu hiyo majira ya kiangazi yaliopita.

Klabu ya Barcelona ikmekuwa ikipambana kuweza kutatua mdororo wa kiuchimu ambao umeikumba klabu hiyo, huku raisi wa klabu hiyo Joan Laporta amekuwa akifanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha klabu hiyo inakuwa sawa kiuchumi.

Joan Laporta, Joan Laporta Kumrudisha Messi Barcelona, Meridianbet

“Nilifanya nililopaswa kufanya ili kuiweka klabu juu zaidi kuliko mchezo bora kwenye historia ya klabu. Namjua Messi tangu akiwa mdogo na namapenda Leo, Barca inampenda leo.

“Kweli ninajihisi mwenye deni kubwa kwa mchezaji bora kwenye historia ya klabu yetu na nitafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha Messi anakuwa na mwisho bora kwenye karia yake akiwa na Jersey ya Barca.

“Ningependa kufanya hivyo. Haitakuwa rahisi, lakini nadhani kwa mipango thabiti, tunaweza kufanya hivyo na tutafanya kadri tuewzavyo ili kuhakikisha messi anakuwa na mwisho bora kwenye karia yake na Barcelona na kushangilia na kila mtu. Alisema Joan Laporta

Messi ametokea kwenye akademi ya Barcelona, na amefanikiwa kucheza kwa mafanikio makubwa kwenye klabu hiyo, huku akicheza michezo 778 na kufungua magoli 672 kwenye mashindano yote na kushinda vikombe 35.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa