Ronaldo: Sihitaji Ballon d'Or Zaidi ya Messi

Cristiano Ronaldo amemjibu mhariri wa France Football ambaye alidai nia pekee ya fowadi huyo wa Manchester United ni “kustaafu akiwa na Ballons d’Or nyingi kuliko Lionel Messi”.

Kupitaia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Cristiano Ronaldo aliamua kukanusha maneno ya mhariri huyo na kusema hiyo siyo nia yake, akimkanusha Pascal Ferré, ambaye alizungumza na New York Times kabla ya tuzo za 2021.

Ferré alinukuliwa na New York Times akisema “Ronaldo ana dhamira moja tu nayo ni kustaafu akiwa na tuzo nyingi zaidi za Ballon d’Or kuliko Messi. Najua kwa sababu ameniambia.”

Hata hivyo, CR7 amekanusha vikali Maneno ya Ferré, akisistiza kuwa haikubaliki kwa mtu aliyehusika kutoa tuzo ya heshima kama hii kusema uwongo kwa njia hii na kuonyesha kutoheshimu mtu ambaye amekuwa akiiheshimu Ufaransa kila wakati.

Cristiano Ronaldo

Kwa hisia kali, Ronaldo amejibu maneno ya Ferré kama alivyonukuliwa hapa chini;

“Matokeo ya leo yanafafanua maoni ya Pascal Ferré wiki iliyopita, aliposema kwamba nilimwambia kwamba dhamira yangu pekee ilikuwa kustaafu na Ballons d’Or nyingi kuliko Lionel Messi”

“Pascal Ferré alidanganya na kutumia jina langu kujitangaza na kukuza uchapishaji wa gazeti ambao anafanyia kazi.”

“Matarajio yangu makubwa katika maisha yangu ya soka ni kutwaa mataji katika ngazi ya klabu na kimataifa, kwa klabu ninazochezea na timu yangu ya taifa.Mmatarajio yangu makubwa katika maisha yangu ya soka ni kuwa mfano bora kwa kila anayetaka”

“Matarajio yangu makubwa katika maisha yangu ni kutaka jina langu liandikwe kwa dhahabu katika historia ya soka duniani.”

“Nitamalizia kwa kusema kwamba mawazo yangu tayari yapo kwenye mchezo ujao wa Manchester United na kila kitu ambacho tunaweza kufikia msimu huu pamoja na wachezaji wenzangu na mashabiki wetu. Kuhusu mengine, mengine ni hayo tu”


 

MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.