Inter Milan wanaripotiwa kukaribia kukamilisha dili la kumsajili Malang Sarr kwa mkopo kutoka Chelsea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa na changamoto ya kupata nafasi kwenye safu ya ulinzi ya Thomas Tuchel msimu huu na amecheza mechi tatu pekee katika michuano yote msimu huu.
Sarr aliwasili Stamford Bridge kutoka Nice mwaka 2020 na mkataba wake na Chelsea ni hadi mwaka 2025, lakini kuondoka klabuni hapo kwa muda kwenda Inter Milan inawezekana.

Kwa mujibu wa SportMediaset, Inter Milan wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo juu ya kumsajili Sarr kwa mkopo mwezi Januari, na mpango huo unatazamiwa kujumuisha kipengele uhamisho wa kudumu.
Inter Milan, mabingwa wa Serie A hawana uhakika juu ya hatma ya mabeki wake wa kati wa sasa Stefan de Vrij na Milan Skriniar, ambao wote wanahusishwa na kuhamia Tottenham Hotspur.
Sarr anadaiwa kuwa na thamani ya €15m (£12.7m) na Chelsea, na amecheza kwa dakika 90 pekee za soka la Premier League msimu huu.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


