Kuibuka kwa virusi vipya cha Covid-19, Omicron variant, kunauwezekano wa kuharibu mchezo wa Young Boys vs Man United.
Timu hizi zinapaswa kuchuana kwenye mchezo wa mwisho wa makundi ya UEFA ifikapo Disemba 8,2021 lakini, kwa mujibu wa hali ilivyo nchini Switzerland, yeyote anayeingia nchini humo akitokea Uingereza, anapaswa kukaa karantini kwa siku 10.
Switzerland sio nchi ya kwanza kuweka mazingira ya tahadhari dhidi ya kirusi kipya cha Covid-19. Uholanzi wameanza kucheza bila ya mashabiki huku pia, mchezo wa West Ham United vs Rapid Vienna ulichezwa bila ya mashabiki kwa sababu za kiusalama.

Endapo itathibitika kuwa United nao wanapaswa kufuata utaratibu uliowekwa kwa raia wengine wote, Uefa watapaswa kutafuta uwanja mwingine na hivyo, mchakato huu, utawaathiri United ambao watapoteza mamilioni ya pesa ambayo wangeyapata kwenye viingilio. Vivyo hivyo kwa Young Boys ambao wanaisaka nafasi ya kucheza Ligi ya Europa.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


