Stars Ugenini dhidi ya Uganda

Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) leo hii watakuwa wageni wa timu ya Uganda kwaajili ya kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya Chan, ambapo mchezo huo utapigwa nchini Uganda.

 

 Stars Ugenini dhidi ya Uganda

Mechi ya kwanza ambayo ilipgiwa hapa nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa Taifa Stars ilipoteza kwa bao 1-0, mchezo ambao mashabiki wa mpira na Taifa Stars walikuwa wakiamini kuwa huo ndio mchezo wao wa kupata alama tatu lakini mambo yakawa tofauti kama ilivyotarajiwa.

Taifa Stars kutupa karata zake ugenini kwa ambapo hapa nyumbani ilishindikana jambo ambalo linahitajika kuwa na utulivu pamoja na kujituma kwa kila mchezaji uwanjani na kutumia kila nafasi wanayoipata uwanjani. Dakika 90 za kipyenga cha mwisho cha refa ndicho kitaamua nani asonge mbele na nani arudi nyumbani akajipange kwa msimu mwingine.

 Stars Ugenini dhidi ya Uganda

Baada ya kupoteza mchezo huo kwa Mkapa, timu ya Taifa ya Tanzania ilimfukuza kocha wake Kim Poulsen kutokana na presha iliyokuwepo ndani na nje ya uwanja. Hivyo kwenye mchezo huu timu itakuwa ikicheza huku ikiwa na benchi la ufundi jipya, ambapo kazi ya ziada itahitajika kwa wote.

Acha ujumbe