Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Imeandika kuwa Kim Poulsen ameondolewa kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” yeye pamoja na wasaidizi wake ambao hawatakuwa sehemu ya benchi la ufundi.

Kim Poulsen Aondolewa Taifa Stars

Aidha, kwenye kikao cha makubaliano baina ya TFF na walimu hao kiliisha kwa makubaliano ya pande zote mbili.

“Pande zote zimefikia makubaliano hayo baada ya kikao, Poulsen ataendelea kubaki katika Timu za Taifa za vijana mpaka mkataba wake utakapomalizika”

Kim Poulsen Aondolewa Taifa Stars

Kwa wakati huu benchi la ufundi la Taifa Stars litakuwa chini ya Kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime pamoja na Makocha wa magolikipa Juma Kaseja.

Kim Poulsen Aondolewa Taifa Stars

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa