Chelsea Namba 1 kwa Usajili

Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza imeongoza kwa kutumia pesa nyingi kwenye usajili msimu huu kwenye majira ya joto, ambapo kwa ujumla imetumia jumla ya $310.2M. Ambapo  kwa ujumla ligi ya Uingereza ndio inaongoza kwa  kutumia  pesa nyingi kwenye usajili kuliko ligi zote tano bora.

Chelsea Namba 1 kwa Usajili

Ligi ya Uingereza imetumia takribani kiasi cha $2.2B ikifuatiwa na ligi ya Italy  Serie A, ambayo imetumia $749.2M, nafasi ya tatu ikishikiliwa na ligi ya Ufaransa ambayo imetumia takribani $558M, Laliga Santander ikitumia kiasi cha $505M na nafasi ya tano ikishikiliwa na ligi ya Ujerumani ambayo wametumia $484.1M.

 

Chelsea Namba 1 kwa Usajili

Chelsea inaongoza kwenye kutumia pesa kwenye usajili huu kutokana na uhitaji wa wachezaji katika maeneo mbalimbali, ambapo kwenye timu kumi zilizotumia pesa nyingi timu za Uingereza zipo 7.

  1. Chelsea $310.2M
  2. Manchester United $261.8M
  3. Westham United $200.2M
  4. Tottenham Hot Spurs $186.9M
  5. Nottingham Forest  $178.1M
  6. Barcelona FC  $168.3M
  7. Psg  $162.2M
  8. Manchester City  $153.4M
  9. Bayern Munchen  $151.2M
  10. Wolveshampton Wonderers $150M

Hizo ni timu kumi zilizotumia pesa nyingi  kufanya usajili katika ligi tano bora Duniani mpaka sasa.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.