Beki na nahodha wa Manchester United, Harry Maguire, ana nafasi kubwa ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Wolves leo usiku.
United watakua Old Trafford kupambana na Wolves katika muendelezo wa EPL leo usiku. Wolves wamekuwa kwenye kiwango bora hasa kwenye idara ya ulinzi. Kwenye takwimu, Wolves ndio timu pekee ambayo haijafungwa magoli mengi ikiongozwa na Manchester City.
Mchezo wa awali, United walishinda kwa goli 1 lakini, mambo yamebadilika. Wolves ya sasa sio ile ya Nuno Espirito Santo. Wanaupiga mwingi!! United pia, wamebadilika kwa kiasi flani, wakilinganishwa na nyakati za Ole Gunnar Solskjaer.

Harry Maguire amepata majeruhi na kuna uwezekano mkubwa akakosekana kwenye mchezo dhidi ya Wolves. Kukosekana kwa Maguire kunapunguza idadi ya wachezaji kwenye idara ya ulinzi.
Victor Lindelof bado yupo karantini, Erick Bailly anajiandaa na mashindano ya AFCON. Hii inamfanya kocha, Ralf Rangnick kubaki na Phil Jones na Rafael Varane kwenye orodha yake. Nani ni nani leo usiku?
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


