Kiungo wa klabu ya Manchester United Carlos Casemiro alietoka klabu ya Real Madrid ya nchini ameanza kuonesha ubora wake ndani ya klabu hiyo baada ya kuanza kwa kusuasua kwa mashetani hao wekundu.
Kiungo huyo anayesifika kwa uwezo wake wa kukaba na kulinda ukuta wake ameonesha ubora wa hali ya juu wakati klabu yake ikishinda dhidi ya Tottenham Hotspurs kwa mabao mawili kwa moja huku kiwango chake alichokionesha jana kikibaki midomoni kwa watu.
Casemiro mshindi mara tano wa kombe la ligi ya mabingwa ulaya ameanza kuingia kwenye mfumo wa kocha Eric Ten Haag kabla ya hapo mwanzo kushindwa kuingia kwenye kikosi huku akiwa akianza kiungo Scott Mctominay lakini tangu ameanza kupata nafasi ameanza kuonesha ubora ambao alikua akiuonesha ndani ya Real ya Madrid.
Kiwango cha Casemiro katika mchezo wa jana dhidi ya Spurs kimekua sehemu ya mazungumzo ya vyombo vya habari na mashabiki wa klabu ya Manchester United wakiona kiwango ambacho walikua wakikitarajia kwa kiungo huyo bora kabisa katika uzuiaji.

