Laporta Apigwa Faini.

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta apigwa faini kutokana na kitendo cha utovu wa nidhamu alichofanya baada ya mchezo kati ya klabu yake dhidi ya Real Madrid katika mchezo uliopigwa wikiendi iliyomalizika katika dimba la Santiago Bernabeu.laportaKatika mchezo ambao Barcelona walipoteza kwa mabao matatu kwa moja baada ya magoli ya Karim Benzema, Federico Valverde, pamoja na Rodrygo Goes huku goli pekee la Barcelona likifungwa na Ferren Torres.

Katika ushindi huo wa jumapili uliiganya klabu ya Real Madrid kuishusha Barcelona ambao walikua wanaongoza ligi kwa tofauti ya magoli na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya alama tatu.laportaRais Laporta alionesha kutoridhishwa na refa wa mchezo huo kutokana na namna alivyochezesha mchezo huku rais huyo akiona hakukua na utata na kuwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya marefa hao wakiongozwa na refa wa kati wa mchezo Jose Maria Sanchez na kuongea maneno yasiyofaa kwa mwamuzi huyo.

Baada ya tukio shishirikisho la mpira nchini Hispania lilikaa kupitia kamati yake na kuamua Laporta atapigwa faini kutokana kitendo alichokifanya ambacho hakikubaliki kwakua ni uvunjifu wa kanuni.

 

Acha ujumbe