Mshambuliaji wa klabu ya Simba Moses Phiri ameahidi kufanya makubwea katika mchezo wa kariakoo derby kati ya klabu yake ya Simba dhidi ya Yanga utakaopigwa siku ya jumapili.
Phiri ambae hakuepo katika mchezo wa Ufunguzi wa ligi kuu msimu ambapo Simba walipoteza mchezo kwa kufungwa magoli mawili yakifungwa na mshambuliaji matata wa klabu ya Yanga Fiston Kalala Mayele.
Mshambuliaji huyo wa Simba Raia wa Zambia ameahidi kufanya vizuri katika mchezo ambapo amesema kama hatafunga basi atasaidia mwezake kufunga huku akitambua kabisa mchezo huo ni mchezo mzito sana lakini yeye amesema atajitahidi kuhakikisha anafanya vizuri katika mchezo huo.Mshambualiaji Moses Phiri amekua na kiwango bora tangu aanze kupata nafasi katika timu hiyo kwani mpaka sasa akiwa amefunga mabao tisa katika michezo tisa hivo wapenzi wa klabu ya Simba wakitarajia makubwa kutoka kwake.