Joan Laporta: Tutaingia Sokoni Januari.

Rais wa klabu ya Fc Barcelona Joan Laporta amezungumza kuhusu klabu hiyo kuingia sokoni katika dirisha dogo la Januari kwajili ya kuboresha kikosi hicho.

Joan Laporta amesema timu hiyo ina mpango wa kuboresha kikosi chao zaidi hivo inatarajia kuingia sokoni mwezi Januari kuangalia namna gani wanaweza kwenda kwenye dirisha hilo na kukiboresha kikosi chao zaidi.joan laportaRais huyo pia amedokeza kabla ya kuingia sokoni watakaa kama bodi ya timu ikiwemo na mwalimu wa klabu hiyo Xavi Hernandez ili kujua mapendekezo yake kwasababu kocha huyo ndo anaweza kutoa mapendekezo kwamba timu imepelea sehemu gani na inatakiwa kuboreshwa sehemu gani.

“Tunalifanyia kazi dirisha la Januari, Tunajadili kama bodi, Xavi na timu yake kwasababu tuna mpango wa kuborsha kikosi chetu kama kawaida” Alisema Joan Laporta.

Klabu ya Barcelona ambayo inafanya vizuri kwenye ligi kuu nchini Hispania ambapo mpaka sasa inaongoza ligi hiyo lakini inaonekana kuteseka kwenye ligi ya mabingwa ulaya ambapo wanakaribia kutolewa kwenye hatua ya makundi.joan laportaKutokana na hali hiyo imewafanya viongozi wa klabu hiyo ikiwemo rais wa klabu kuna ulazima wa kurudi sokoni kufanya maboresho ya klabu hiyo ili kuifanya kua shindani zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.