Golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer ameonyesha kufarijika kwamba timu yake ya Taifa bado ipo hai katika Kombe la Dunia baada ya kupata sare ya 1-1 kwenye mchezo wao wa jana dhidi ya Hispania.

Matumaini ya Ujerumani kufuzu hatua ya 16 yamepata pigo la kushangaza baada ya kuanza kwa kupoteza mechi yao ya kwanza dhidi ya Japana kwa mabao 2-1, lakini pia jana pia wakashindwa kupata ushindi.
Wakati huo huo kwenye Kundi hilo baada ya Costa Rica kucharazwa kwa mabao 7-0 dhidi ya Hispania ilijibu kichapo hicho kwa kuifunga Japan 1-0 na kumuacha Ujerumani ashikilie mkia Kundi E.
Alvaro Morata ndiye aliyeitanguliza mbele Hispania kwa kupachika bao moja katika uwanja wa Al Bayt, lakini Nicklas Fullkrug wa Ujerumani alitoka kwenye benchi na kusawazisha na kupata pointi ya kwanza ya timu yake.

Ili Neuer na wenzake wafuzu hatua ya 16 bora lazima iifunge Costa Rica katika mechi ya mwisho ya kundi hilo siku ya Alhamisi huku pia akitarajia Japan afungwe na Hispania. Mlinda mlango Neuer anafuraha kwamba Taifa lake bado lina nafasi ya kuepuka kutolewa kwa mara ya pili mfululizo kwa Kombe la Dunia katika hatua ya makundi.
Neuer amesema kuwa; “Ilikuwa mechi ngumu dhidi ya timu nzuri sana ya Uhispani tulipambana na hatukuruhusu nafasi nyingi kwa dakika 90 na kazi yetu ya ulinzi ilikuwa nzuri sana kutoka mbele hadi nyuma.”
Golikipa huyo aliendelea kusema kuwa jambo kuu ni kwamba bado wako hai, kitu ambacho wanaweza kuwa na ushawishi juu yake ni kupata pointi tatu dhidi ya Costa Rica.
Fullkrug alicheza mechi yake ya kwanza ya Kimataifa mwanzoni mwa mwezi huu na kufunga bao lake la kwanza la ushindani akiwa na Ujerumani katika mwonekano wa kipekee baada ya kuchelewa kuitwa kwenye kikosi.

Mshambuliaji huyo wa Werder Bremen mwenye umri wa miaka 29 naye akasema kuwa walidhamiria kupata matokeo kutoka kwa mchezo, na ilikuwa muhimu sana kujiamini, bado wana nafasi ya kuimarika na hawahitaji kubebwa, lakini wanaweza kwenda kwenye mchezo wa fainali wakiwa na matumaini kwamba wanaweza kufanikiwa.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


