Manuel Neuer Kuendelea Kukosekana Tena Leo.

Kipa namba moja wa klabu ya Fc Bayern Munich Manuel Neuer ataendelea kukosekana tena leo klabu hiyo ikenda kumenyana na klabu ya Freiburg baada ya kusumbuliwa na majeraha ya bega.manuel neuerGolikipa huyo ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ataendelea kuugulia maumivu kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya klabu ya Freiburg kutokana na majeraha ya bega aliyoyapata siku kadhaa nyuma yaliyomfanya kukosa pia mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya katikati ya wiki katika ushindi wa magoli manne kwa mbili.

Lakini kocha wa klabu hiyo Nagelsman anaamini Manuel Neuer anaweza kurejea katika mchezo wa jumanne wa DFB Pokal kati yao na klabu ya Augsburg.

“Manuel Neuer hatacheza. bado ana maumivu. Natumaini atarejea wiki ijayo, Lakini Freiburg inaweza kua mapema sana kwake” Kocha huyo alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea hali nahodha wake.

“Bila dawa za kutuliza maumivu, Hawezi kusogeza bega kwa njia ambayo inaruhusu mchezo. Haina maana ya kumsukuma acheze kila mchezo”manuel neuer“Nafikiri ataweza kucheza tena wiki ijayo huko Augsburg. Hiyo inanudhi lakini ndivyo ilivyo” Kocha Nagelsman akielezea hali ya kipa wake namba moja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.