Vipers Yaitoa Tp Mazembe Yatinga Makundi Kibabe.

Klabu ya Vipers na mabingwa wa soka nchini Uganda wamefanikiwa kuwatupa nje Tp Mazembe kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.vpersVipers wamefanikiwa kuwatoa Tp Mazembe katika arghi ya nyumbani katika mchezo wa pili wa hatua ya kwanza ya ligi mabingwa Afrika baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bila kufungana na kuamuliwa kwa mikwaju ya penati na klabu hiyo kutoka nchini Uganda ikafanikiwa kushinda kwa mikwaju 4-2 dhidi ya Mazembe.

 

Ikumbukwe mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Uganda wiki iliyopita uliisha kwa sare ya bila kufungana pia huku klabu ya Tp Mazembe wakionekana kupewa nafasi zaidi kuelekea mchezo wa pili ambao walikua wanaenxca kuucheza katika uwanja wao wa nyumbani lakini mambo yamekua tofauti.

Timu ya Vipers imekua na kiwango bora baada ya kubeba ubingwa wa ligi kuu nchini Uganda na kujenga kikosi cha ushindani chini ya kocha raia wa Brazil Roberto Oliveira na inawafanya kua timu ya kuangalia zaidi kutoka ukanda wa Afrika mashariki baada ya Simba ambao wamekua na kawaida ya kufuzu hatua ya makundi kutoka ukanda huu.vipersHuu ni msimu wa pili wa klabu ya Tp Mazembe kutolewa katika hatua ya kwanza na kuangukia katika kombe la shirikisho kama ambavyo walitolewa msimu 2020/21, Jambo hili limewafanya watu kuanza kufikiria labda ndo mwisho wa zama za klabu hiyo kongwe na yenye mafanikio kutoka Congo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.