Ronaldo de Lima staa wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil pamoja na vilabu vya Real Madrid,Barcelona pamoja na Inter Milan amefichua kwasasa yupo kwenye matibabu ya msongo wa mawazo.Staa huyo amesikitishwa na watu wengi wanapopuuza matatizo ya afya ya akili wakati wakicheza mpira.
Mshambuliaji huyo mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tatu na watu wakimtambua kama mshambuliaji bora kabisa wa kizazi chake ambaye amepita vilabu vikubwa na kufanya makubwa na timu ya taifa ya Brazil.
Wakati wa uzinduzi filamu ya Ronaldo maarufu iliyofanyika nchini Hispania ndipo gwiji huyo alipofunguka na kueleza yaliyomkuta mchezaji huyo “Leo niko kwenye matibabu. Nimekua kwenye matibabu miaka miwili na nusu, Na najiskia vizuri sasa kuliko hapo awali. Lakini basi tena mimi ni kutoka kwenye kizazi ambacho ulitupwa uwanjani na ilipidi ufanye bidii bila drama hata kidogo”
“Ninaangalia nyuma na naona ndio, Tulikua na shida kubwa ya akili tena bila maandalizi ya aina yeyote”Ronaldo amesisitiza kizazi hichi ni tofauti na kile walichokua wao kwani wachezaji wasasa wamejiandaa na tatizo la afya ya akili.
Mshambuliaji maarufu kama El Fenomeno anaeleza kwa kipindi kile ilikua ngumu kugundua kwamba mtu una tatizo hilo na lilipuuzwa pia jambo ambalo liliwafanya wengi kuathirika na tatizo hilo ikiwemo yeye mwenyewe japo kwasasa anaendelea vizuri.

