Kiungo wa klabu ya Fc Barcrlona na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie de Jong amesema rais wa klabu hiyo Joan Laporta alikua anamshinikiza aondoke klabuni hapo lakini yeye hakua na moango wa kuondoka.
Kiungo huyo ambaye alikua anahusishwa kuondoka klabuni hapo kwa takribani kipindi kizima cha dirisha la usajili tena akihisishwa zaidi na klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza ambayo inafundishwa na Mholanzi mwenzake De jong bwana Eric Ten Haag.
Watu wengi walifikiri Frenkie de Jong angeungana na mwalimu wake katika klabu ya Ajax lakini kiungo huyo aliamua kubaki kwenye klabu ya Barcelona.
Kiungo huyo wa kati amedai alikua anajua kwa kiasi klabu hiyo ilikua inataka aondoke klabuni hapo lakini yeye hakua na mpango huo na aliendelea kua mtulivu kwakua lengo lake ilikua sio kuondoka klabuni hapo.
“Nilikua mtulivu. Niliamua mwezi Mei kwamba nataka kubaki. Mawazo yangu hajayawahi kubadilika kwa kipindi chote hiki, Nilibaki kua mtulivu” Alisema Frenkie de Jong akiiambia tovuti ya Ziggo juu ya msimamo wake ulivyokua wakati rais na klabu kwa ujumla vikimshinikiza aondoke klabuni hapo.
Kiungo pamoja na kubaki klabuni hapo lakini amekua akipata nafasi mara chache sana kwenye kikosi hicho chini ya kocha Xavi huku akiwa ameanza kwenye michezo minne tu msimu huu na taarifa zikieleza anataka kuondoka klabuni hapo kwasasa.

