Kiungo wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie De Jong inaelezwa anafikiria kuondoka katika klabu hiyo kama hali ya kutopata nafasi kwenye kikosi hicho chini ya mwalimu Xavi itaendelea.
Kiungo huyo ambaye alikua anawindwa zaidi na klabu ya Manchester United kwenye dirisha lililopita kwa zaidi ya miezi mitatu na kuamua kusalia klabuni hapo,Lakini hali imekua tofauti kwani kiungo huyo amekua sio chaguo la kwanza ndani ya timu hiyo jambo linalomfanya afikirie kutimka klabuni hapo.
Frenkie De Jong amekua hafurahishwi na hali ya kukaa benchi kwenye timu hiyo mara kwa mara na kufikiria kuondoka klabuni hapo kwenda kutafuta nafasi kwenye timu nyingine na taarifa zinaeleza kama hali hii itaendelea basi kiungo huyo anaweza kuomba kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha dogo Januari.
Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi amekua akiwatumia zaidi viungo watatu wa kihispaniola Sergio Busquets,Pedri, pamoja na Gavi kitu ambacho kinamfanya Frenkie De Jong kukosa nafasi kwenye timu hiyo ya Catalan.
Pia kiungo huyo wa kiholanzi pia anahofia kukosa nafasi kwenye cha timu ya taifa ya Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu.

