Ronald Araujo Anaendelea Vizuri Baada ya Upasuaji.

Beki wa klabu ya Barcelona Ronald Araujo amethibitisha kwamba yupo kwenye kipindi cha kupona baada ya kufanyiwa upasuaji wa paja katika wiki kadhaa zilizopita.ronald araujoBeki huyo raia wa Uruguay ambaye siku kadhaa nyuma zilitoka taarifa kua atafanyiwa upasuaji baada ya kupata shida kwenye paja lake amethibitisha kukamilisha upasuaji wake salama na anaendelea vizuri kwasasa.

Ronald Araujo ambaye baada ya kufanyiwa upasuaji huo inaelezwa atakua nje ya uwanja kwa takribani wiki 10 hadi 12 jambo ambalo litamfanya kukosa michuano ya kombe la dunia na timu yake ya taifa ya Uruguay ambapo koicha atataja wachezaji 23 wa mwisho kuelekea michuano hiyo inayoanza mwezi Novemba mwaka huu pale Qatar.

Kuna taarifa zilitoka wiki kadhaa nyuma zikieleza timu ya taifa ya Uruguay ilikua ikishikinikiza klabu ya Barcelona kuchelewesha upasuaji huo ili waweze kumpata beki huyo kwenye kikosi chao kitakachoenda Qarar lakini ilishindikana.ronald araujoKupitia mtandao wake wa kijamii wa Tweeter Ronald Araujo aliandika “Baada ya wiki kali, Nataka kuwaambia nyinyi  kwamba, Namshukuru na kila kitu kilenda sawa wakati wa upasuaji. Tayari nimeanza kupona, Ninalenga kurudi kwa njia bora zaidi. Asanteni nyote kwa jumbe zenu za ushikirikiano” Aliandika beki huyo kwenye ukurasa wake wa kijamii.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.