Ronaldo Akanusha Kumtolea Maneno Machafu Kocha Wake Fernando Santos

Cristiano Ronaldo amekanusha kumtolea maneno machafu kocha wake Fernando Santos na kudai kuwa kauli yake ilielekezwa kwa mchezaji wa Korea Kusini ambaye alimwambia ‘anyamaze’ wakati Ureno ilipochapwa 2-1 kwenye fainali ya Kundi H.

 

ronaldo

Ronaldo alikanusha kabisa kumkalipia Fernando Santos alipofanyiwa mabadiliko wakati wa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Korea Kusini kwenye Kombe la Dunia siku ya Ijumaa, timu zote zikitinga raundi inayofuata.

Ronaldo, nahodha wa Ureno, alisema maneno aliyotoa wakati akitoka uwanjani dakika ya 65 yalimlenga mchezaji wa Korea Kusini.

Vyombo vya habari vya Ureno vilisema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na Juventus, ambaye aliachana na klabu hiyo ya Uingereza mwezi uliopita, alionekana kumpinga Santos kuhusu uamuzi wa kumbadilisha, akitumia lugha chafu dhidi ya kocha huyo.

 

ronaldo

“Kilichotokea ni kabla ya kubadilishwa kwangu, mchezaji wa Korea Kusini aliniambia nitoke haraka. Nilimwambia anyamaze kwani hana mamlaka hayo. Hakukuwa na kutofautiana (na kocha),” Ronaldo alinukuliwa akisema na waandishi wa habari wa Ureno.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anatafuta kufikia rekodi ya Ureno ya mabao mengi zaidi ya Kombe la Dunia inayoshikiliwa na Eusebio, ambaye alifunga mabao tisa mwaka wa 1966 nchini Uingereza, michuano pekee ya Kombe la Dunia aliyocheza.

 

ronaldo

Santos, alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la kubadilisha mchezaji wa benchi, pia alisema mchezaji wa Korea Kusini amekuwa mkali katika maoni yake kuelekea mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or.

“Niliona mwingiliano na mchezaji wa Korea na sina shaka juu ya kile kilichotokea,” Santos alisema.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.