Pele Atatumia Krismasi Hospitalini Baada ya Kupata Saratani

Saratani ya Pele imeongezeka na nyota huyo wa Brazil atatumia Krismasi akiwa hospitalini kuangalia afya yake.

 

Pele Atatumia Krismasi Hospitalini Baada ya Kupata Saratani

Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia ametumia wiki tatu zilizopita katika Hospitali ya Israelta Albert Einstein mjini Sao Paulo. Pele amekuwa na saratani ya utumbo mpana tangu 2021 na aliondolewa uvimbe mnamo Septemba mwaka huo.

Amekuwa akitibiwa mara kwa mara na ripoti kutoka hospitalini siku ya Jumatano ilisema kwamba anahitaji huduma ya ziada inayohusiana na matatizo ya figo na moyo.

Pele mwenye umri wa miaka 82 atakuwa hospitalini kwa ajili ya Krismasi, bintiye Kely Nascimento alifichua kwenye mitandao ya kijamii. Katika mtandao wa Instagram, aliandika: “Krismasi yetu nyumbani imesimamishwa.”

Pele Atatumia Krismasi Hospitalini Baada ya Kupata Saratani

“Tuliamua na madaktari kwamba, kwa sababu mbalimbali, ingekuwa bora kwetu kukaa hapa kwa uangalifu wote ambao familia hii mpya huko Einstein inatupa, mapenzi yako kwake, hadithi zake na maombi yake ni faraja kwasababu tunajua hatuko peke yetu.”

Ripoti ya hospitali hiyo ilisema Edson Arantes do Nascimento [Pele] anaonyesha kuendelea kwa ugonjwa huo wa saratani na anahitaji uangalizi mkubwa zaidi kuhusiana na matatizo ya figo na moyo.

Pele Atatumia Krismasi Hospitalini Baada ya Kupata Saratani

“Mgonjwa anasalia hospitalini katika chumba cha kawaida, chini ya uangalizi muhimu wa timu ya matibabu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.