Scott Parker amerejea kwenye uongozi baada ya kutimuliwa na Bournemouth na kuchukua udhibiti kwenye klabu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Club Brugge’.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa hana kazi tangu atemwe na Bournemouth mwishoni mwa Agosti.
Kichapo cha 9-0 dhidi ya Liverpool kilithibitisha kuwa mwisho kwa Parker baada ya Bournemouth kupoteza mechi tatu kati ya nne za mwanzo za Ligi ya Premia.
Na kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya uchezaji kama mchezaji au meneja, Parker ameamua kufanya majaribio nje ya nchi baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa Brugge ya Ubelgiji.
Brugge iliachana na kocha wao mkuu wa awali Carl Hoefkens mapema wiki hii huku klabu hiyo ikishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ubelgiji Pro League.
Hoefkens alikuwa amechukua usukani msimu wa joto, lakini amedumu kwa miezi sita pekee – licha ya kumuongoza Brugge katika hatua ya mtoano ya Kombe la Uropa kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Klabu ya Brugge, ambao wameshinda taji la ligi kuu kwa misimu mitatu iliyopita, walimtangaza Parker kama bosi wao ajaye Jumamosi alasiri.
Taarifa ilifichua kuwa kiungo huyo wa zamani wa Tottenham na Chelsea atawasilishwa rasmi wiki ijayo.
Ilisomeka hivi: “Scott anamrithi Carl Hoefkens kama kocha mkuu wa Club Brugge.
“Mnamo Februari 2018, Parker alikua kocha mkuu katika Craven Cottage.
“Mnamo 2020 alipanda daraja hadi Ligi kuu ya Uingereza akiwa na Londoners. Baada ya kucheza Fulham, Parker alijiunga na Bournemouth.
“Parker pia aliweza kulazimisha kupanda Ligi Kuu akiwa na The Cherries.
“Scott atawasilishwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Belfius Basecamp.”
Mechi inayofuata ya Brugge ni pambano ugenini dhidi ya viongozi wa ligi Genk Jumapili ijayo, ambao wako mbele kwa alama 12 kwenye msimamo.
Genk wamepoteza mechi mbili pekee kati ya 18 za mwanzo, na wanajivunia rekodi bora zaidi ya ulinzi nchini Ubelgiji.
Scott bila shaka atakuwa akifurahia changamoto ya mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa, Brugge atamenyana na Benfica katika hatua ya 16 bora Februari 15.

