Scott Parker aliekua kocha Afc Bournamouth amefutwa kazi na waajiri wake hao wa zamani na kumfanya kua kocha wa kwanza kufutwa kazi msimu huu ndani ya ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Afc Bournamouth imefikia hatua ya kumfuta kazi kocha huyo ni baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo ya Epl dhidi ya vilabu vya Manchester City,Arsenal, na Liverpool ambao mchezo huu ndo umekua chachu ya kufukuzwa kwake baada ya kupokea kipigo kizito cha magoli tisa kwa bila hivo kupelekea mabosi wa klabu hiyo kumfuta kazi kiungo huyo wa zamani wa Fulham.

scott parker

Scott Parker ambae amepambana kuipandisha timu hiyo daraja kutoka daraja la pili maarufu kama Championship na kuipandisha ligi kuu  baada ya kuachana na klabu yake ya zamani alikua anaitumikia ya Fulham na sasa kocha anaweka rekodi ya kua kocha wa kwanza kufukuzwa kwenye msimu huu wa 2022/23 wa ligi kuu ya Uingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa