Ligi kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa michezo miwili, ambapo mchezo wa mapema kabisa utakuwa kati ya Geita Gold dhidi ya Polisi Tanzania majira ya saa 10:00 jioni.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Nyankumbu huku timu zote zikitafuta pointi 3 ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo kwenye ligi kuu.
Geita wapo nafasi ya 5 baada ya kucheza michezo 20, wakiwa wameshinda mechi zao sita, sare tano na kupoteza michezo mitano, wakijikusanyia pointi zao 27 hadi sasa kwenye Ligi.

Wakati kwa upande wa Polisi Tanzania wapo nafasi ya mwisho kwenye msimamo baada ya kuvuna pointi zao 14 kwenye michezo 20 waliyocheza, wakiambulia ushindi mara 3, sare 5 na vipigo 12.
Mechi zilizopita za timu hizo mbili wote walishinda, lakini mechi tatu za mwisho kukutana kati yao Wachimba Madini wameshinda zote. Kesho Polisi atakubali kichapo tena?

