Mchezo mwingine wa ligi kuu kesho utakuwa kati ya Kagera Sugar ambaye atakuwa nyumbani kumualika Coastal Union ya Tanga majira ya saa 1:00 usiku.

Coastal Union wapo nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi zake 20, na kuvuna alama 18 hadi sasa, wakiwa wameshinda michezo yao minne, sare sita na kupoteza michezo 10 kwenye ligi.
Wakati vijana wa Mecky Mexime wao wanashikilia nafasi ya 8 pointi zao 24 kibindoni, ushindi mara sita, sare sita na kupoteza michezo jumla ya nane baada ya kucheza michezo yao 20.

Kagera ametoka kudondosha pointi sita kwenye michezo yake miwili iliyopita, huku Coastal wao wakitoka kutoa sare mechi zao mbili zilizopita.
Mechi ya mwisho kumenyana timu hizi mbili, Wagosi wa Kaya waliondoka na pointi tatu wakiwa nyumbani.

