Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani imekamilisha usajili wa golikipa wa Borussia Monchengladbach Yann Sommer.

Sommer atatia saini mkataba unaotumika hadi Juni 2025 kwa kuwa vipimo vya afya tayari vimeshafanyiwa kazi juu ya mlinda mlango huyo..
Bayern watalipa €8m pamoja na nyongeza za €1.5m, kama alivyoripoti Blick Yann Sommer atafanyiwa vipimo na kisha kutambulishwa kama mbadala wa Manuel Neuer ambaye aliumia baada ya kutoka kombe la Dunia.

Klabu hiyo ambayo ipo chini ya kocha Julian Nagelsmann wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza baada ya Kombe la Dunia hapo kesho dhidi ya Rb Leipzig huku Munich wakiwa kileleni mwa msimamo.

