Kiungo wa klabu ya Simba Saidoo Ntibazonkiza atakosekana katika mchezo wa kwanza wa makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya klabu ya Horoya Fc ya nchini Guinnea.
Saidoo Ntibazonkiza atakosekana katika mchezo utakaopigwa nchini Guinnea kati ya Horoya Fc dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika, Kwani mchezaji huyoo amepata majeraha ya nyama za paja katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars hivo hataweza kuwepo kwenye kikosi hicho.
Kuthibitisha hilo mchezaji huyo hajaonekana katika msafara wa wachezaji wa Simba waliosafiri kuelekea nchini Guinnea mapema Alfajiri ya leo, Hivo ni wazi kiungu huyo mshambuliaji atakosa mchezo huo akiungana na Augastine Okrah.
Saidoo Ntibazonkiza baada ya majeraha yake katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars kiungo huyo alishindwa kufanya mazoezi vizuri na wenzake, Lakini taarifa zinaeleza mchezaji huyo anaendelea vizuri lakini hataweza kushiriki mchezo wa jumamosi kwasababu bado hajawa fiti kwa asilimia 100.
Kiungo Ntibazonkiza amekua kwenye kiwango bora tangu ajiunge na klabu ya Simba kwenye dirisha dogo la mwezi Januari akitokea klabu ya Geita Gold, Hivo ni wazi litakua pengo kubwa kwa klabu ya Simba kuelekea mchezo huo kutokana na ubora ambao kiungo huyo kauonesha siku za karibuni.

