Ripoti nyingi nchini Italia zinadai kuwa Inter haitawatoza faini Romelu Lukaku na Nicolò Barella baada ya mabishano ya uwanjani dhidi ya Sampdoria siku ya Jumatatu.

Magazeti ya Gazzetta dello Sport na Calciomercato.com yanadai Nerazzurri wameamua kutowatoza faini wachezaji hao ambao walilaumiana hadharani na kutukanana katika kipindi cha kwanza cha sare ya 0-0 dhidi ya Sampdoria huko Marassi Jumatatu usiku.
Kulingana na ripoti hizo, Lukaku na Barella walisafisha hewa kwenye uwanja wa mazoezi wa Inter siku ya jana wakati wakurugenzi wa vilabu walipokutana na timu na wafanyakazi, akiwemo kocha Simone Inzaghi.
Inaripotiwa kuwa wakuu wa klabu hiyo hawajafurahishwa na tabia ya Lukaku na Barella lakini hawatachukua hatua kwa sababu wametatua masuala yao ndani.

Wakurugenzi wa Inter hawataki kusababisha mvutano zaidi ndani ya chumba cha kubadilishia nguo lakini wanatarajia kutoona kitu kama hicho katika siku zijazo.
Kulingana na Gazzetta, Inter haitakubali tabia kama hiyo kutoka kwa mchezaji wao yeyote katika siku zijazo, haswa Barella, ambaye mara nyingi amekuwa akionekana kuwalaumu wachezaji wenzake uwanjani msimu huu.

