Klabu ya Manchester imemuongezea mkataba mpya beki wake wa kushoto muhimu klabuni hapo raia wa kimataifa wa Uingereza Luke Shaw, Beki huyo ameongezewa mkataba wa miaka minne wa kuendelea kusalia viunga vya Old Trafford.
Luke Shaw ni miongoni mwa wachezaji ambao walikua wanahitajika kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi, Kwani beki huyo yupo kwenye mpango wa muda mrefu wa kocha wa klabu hiyo kwasasa Erik Ten na ndio sababu ya beki huyo kuongezewa mkataba mpya.
Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua kwenye kiwango bora sana chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Erik Ten Hag, Hivo kocha huyo alipendekeza beki huyo kuongezewa mkataba ili aendelee kusalia ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.
Luke Shaw ambaye alikua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara lakini msimu huu hali imebadilika kwasababu majeraha hayajakua sehemu ya maisha yake na kufanya beki huyo kuonesha kiwango bora sana ndani ya klabu ya Manchester United.
Manchester United mpaka sasa inafanya mazungumzo na wacheaji wake muhimu ili kuweza kuwaongezea mkataba kama ambavyo wamefanya kwa Luke Shaw, Kwani kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag yuko kwenye mpango wa kusuka timu yenye ushindani mkubwa na kwa muda mrefu.

