Mlinda mlango wa zamani wa Real Madrid, Iker Casillas amewachoma Juventus katika mahojiano ya hivi majuzi na kusema kuwa ni ‘nzuri kwa soka la Italia’ timu nyingine zimeanza kukomesha ubabe wao wa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Mhispania huyo aliiambia DAZN katika kipengele cha hivi majuzi kwamba amekuwa akifurahia kutazama calcio ya Italia, lakini alifikiri kwamba Serie A imekuwa yakuchosha’ wakati timu moja tu ilikuwa ikishindania ubingwa kila mwaka.
Casillas aliwaambia watazamaji: “Niliipenda Serie A sana nilipokuwa mdogo, hasa ilipochukuliwa kuwa ligi bora zaidi duniani. Wachezaji wakubwa wote walicheza hapo. Ukweli ni kwamba Serie A ilipitia kipindi ambacho ni Juventus pekee ndiyo walishinda na ikawa ya kuchosha, lakini sasa ukweli kwamba Napoli, pamoja na Inter na Milan katika miaka ya hivi karibuni wamesimamisha utawala wa Juve na hiyo ni nzuri kwa soka la Italia.”
“Je, nimewahi kufikiria kuhusu kucheza Serie A? Kusema ukweli, ndiyo, ninaheshimu sana timu zote, lakini Real Madrid ni Real Madrid.”

Bianconeri walishinda mataji tisa mfululizo kati ya msimu wa 2010-11 na 2019-2020. Inter chini ya Antonio Conte iliwazuia kushinda mara 10 mfululizo, kabla ya Milan ya Stefano Pioli kushinda scudetto mara ya mwisho.
Sasa, inaonekana hakika kwamba Napoli itatwaa kombe hilo mwishoni mwa msimu huu. Hakujawa na washindi watatu tofauti wa Serie A ndani ya miaka mitatu tangu Lazio, Roma na Juve kila moja ichukue ubingwa katika misimu kati ya 2000 na 2002.

Mara ya mwisho kwa timu nne tofauti kushinda Serie A ndani ya miaka minne ilikuwa kati ya misimu ya 1988-89 na 1991-92, ambapo Inter, Napoli, Sampdoria na Milan zilishinda ubingwa mmoja kila moja.

