Ancelotti: Nina Imani Nitakuwepo Madrid Msimu Ujao

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kua ana matumaini makubwa ataendelea kuinoa klabu hiyo kwa msimu ujao kwakua anaamini rais wa klabu hiyo Florentino Perez anataka aendelee kubaki klabuni hapo.

Kocha Ancelotti amekua akihusishwa kuondoka klabuni hapo mara kwa mara msimu huu taarifa zikieleza anaweza kuondolewa kutokana na mwenendo uliopo wa klabu hiyo, Lakini taarifa zikieleza kocha huyo anaweza kutimkia timu ya taifa ya Brazil ambayo imekua ikimfuatilia kwa muda mrefu.ancelottiKocha huyo raia wa kimataifa wa Italia amekua hana muenendo mzuri sana ndani ya klabu hiyo kwani mpaka sasa ameachwa mbali na wapinzani wao klabu ya Barcelona kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania, Lakini wakionekana kupoteza michezo mbalimbali kwenye hali ya kushtusha.

Carlo Ancelotti alifanikiwa kufanya makubwa msimu uliomalizika baada ya kurejea klabuni hapo tangu mwaka 2015, Akifanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya na taji la ligi kuu ya Hispania La liga na kutokana na mafanikio hayo ndani ya klabu ni jambo ambalo linaendlea kumpa imani kocha huyo.ancelottiLicha ya tetesi zinazoeleza kua kocha Ancelotti anaweza kutimuliwa ndani ya timu lakini kocha huyo ameonesha kutokua na wasiwasi baada ya kuongea na waandishi wa habari mapema, Kwani anaamini ana ushirikiano mkubwa kutoka kwa rais wa klabu hiyo Florentino Perez.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.