Terzic: Dortmund Inakaribia Ubingwa wa Bundesliga Kuliko Hapo Awali

Kocha mkuu wa Borussia Dortmund, Edin Terzic anataka wachezaji wake kufaidika na nafasi yao katika mbio za ubingwa wa Bundesliga, akisema wako karibu zaidi kuliko hapo awali.

 

Terzic: Dortmund Inakaribia Ubingwa wa Bundesliga Kuliko Hapo Awali

Tangu Dortmund kutwaa mataji mawili mfululizo ya ligi kati ya 2010 na 2012, wapinzani wao Bayern Munich wametawala, na kubeba taji hilo kwa kampeni 10 mfululizo.

Hata hivyo, mwenendo mzuri wa kiwango bora tangu kuanza kwa 2023 ambapo wamepoteza mchezo mmoja pekee wa Bundesliga dhidi ya Bayern, unamaanisha kuwa Dortmund wako pointi mbili pekee nyuma ya timu hiyo ya Bavaria wakiwa na mechi sita za kucheza.

Akiwa na nafasi ya kweli ya kumaliza mfululizo wa mataji ya Bayern, Terzic anatumai timu yake inaweza kuchukua fursa hiyo, akiwaambia waandishi wa habari kabla ya mchezo wa hapo kesho dhidi ya Eintracht Frankfurt: “Tuko karibu zaidi kuliko hapo awali kwa kombe la ubingwa, na hatutaki kukosa nafasi hii. Tunapaswa kuanza kunyakua nafasi hii na kila kitu tulichonacho haraka iwezekanavyo, ili kiwe kweli.”

Terzic: Dortmund Inakaribia Ubingwa wa Bundesliga Kuliko Hapo Awali

Ikiwa tunataka kufanikiwa, sote tunapaswa kuwa tayari kwenda hatua ya ziada. Tunapaswa kuwekeza kila kitu ili kutumia nafasi yetu ya kuanzia. Ili kufanya hivyo, tunahitaji ushindi wa nyumbani hapo kesho. Alisema kocha huyo.

Dortmund wangekuwa sawa kwa pointi na Bayern kama si kwa kuruhusu bao la kusawazisha dakika ya 97 wakiwa ugenini dhidi ya Stuttgart ambao walikuwa pungufu mara ya mwisho, na Terzic anahisi wachezaji wake wanaelekea katika hatua ya mwisho ya kampeni.

Terzic: Dortmund Inakaribia Ubingwa wa Bundesliga Kuliko Hapo Awali

Terzic pia alifichua kuwa kulikuwa na alama ya kuuliza juu ya uwepo wa Niklas Sule, Nico Schlotterbeck na Anthony Modeste kwa pambano dhidi ya Frankfurt inayowinda kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa alisema kuwa tayari waliweza kuongeza nguvu kwenye mazoezi kwahiyo wanasubiri na kuona.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.