Winga wa zamani wa klabu ya Liverpool anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani Sadio Mane inaelezwa kufukuziwa na mashetani wekundu klabu ya Manchester United kuelekea kufunguliwa kwa dirisha kubwa.
Klabu ya Bayern Munich inaelezwa itamuweka sokoni Sadio Mane kwenye dirisha kubwa lijalo kutokana na kua winga huyo wa kimataifa wa Senegal hayupo kwenye mipango ya kocha wa sasa wa klabu hiyo Thomas Tuchel, Hivo Manchester United inamuhitaji winga ili kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji.
Sadio Mane ambaye amekua hana msimu mzuri ndani ya klabu ya Bayern Munich tangu apate majeraha kabla ya michuano ya kombe la dunia, Kitu ambacho kimemfanya kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza ndani ya klabu ya Bayern Munich na kufikiria kumuuza staa huyo.
Manchester United haitakua peke yake katika mbio za kumuwania winga huyo kwani staa huyo anawaniwa pia na matajiri wa klabu ya Newcastle United, Hivo mchuano ni mkali kati ya Magpies na mashetani wekundu ambao wote wameonesha nia ya kuhitaji saini ya mchezaji huyo.
Inafahamika klabu ya Manchester United inataka kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji ambayo imeonekana kutokufanya vizuri na mchezaji kama Mane ambae amekua na kiwango bora sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza wanaona inaweza kua karata nzuri kwa upande wao.

