Klabu ya Manchester City leo itashuka dimbani kuikaribisha Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya utakaopigwa katika dimba la Etihad usiku wa leo.
Manchester City kwenye msimu bora kabisa wanaonekana kufukuzia rekodi ya kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja, Kwani mpaka sasa wako kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, wametinga hatua ya fainali ya ligi ya kombe la FA, Vilevile wakiwa kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya hivbo wakifanikiwa kushinda leo watakua wamejiweka kwenye nafasi nzuri zaidi.
Vijana hao wa Pep Guardiola wanakabiliwa na mchezo mgumu zaidi leo dhidi ya miamba ya soka nchini Hispania klabu ya Real Madrid, Lakini endapo watafanikiwa kuwatupa nje vigogo hao kwenye mchezo wa leo basi watakua na nafasi nzuri zaidi ya kutimiza ndoto zao.
Klabu ya Manchester United ndio klabu pekee kutoka nchini Uingereza kuweza kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja ikijumuisha na taji la ulaya ambapo walifanya hivo mwaka 1999, Lakini Manchester City wanaonekana wanaweza kufanya ambacho walikifanya mahasimu wao miaka 23 iliyopita.
Pep Guardiola yeye kwa upande wake anafukuzia rekodi ya kutwaa taji la tatu la ligi ya mabingwa ulaya baada ya kutwaa taji hilo akiwa na Fc Barcelona mara mbili, Lakini pia kurudia rekodi ya Treble kwa maana ya kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja kitu ambacho alikifanya ndani ya Barcelona mwaka 2009.

