Xaka Kutimka Arsenal Mwishoni mwa Msimu

Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uswisi Granit Xaka anatarajia kutimka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takribani miaka saba sasa.

Granit Xaka amekua mchezaji alieitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu lakini inaonekana ni kama safari inaelekea ukingoni, Kwani inaelezwa mchezaji huyo ana mpango wa kutimka kabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na kuelekea nchini Ujerumani ambapo alitokea kabla ya kujiunga na washika mitutu hao wa London.xakaTaarifa za awali kutoka ndani ya Arsenal zilieleza klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na kiungo huyo wa kimataifa wa Uswisi ili kumuongezea mkataba wa kuendelea kubakia ndani ya timu hiyo, Lakini mpaka sasa hamna dalili za kiungo kuongezewa mkataba mpya.

Klabu ya Bayern Leverkusen inaelezwa imeshafanya mazungumzo na Xaka na imeandaa fungu la paundi milioni 15 ili kumng’oa kiungo huyo ndani ya viunga vya Emirates, Huku kiungo huyo akitarajiwa kusaini mkataba mrefu wa miaka minne ina maana dili hilo likifananikiwa atakua ndani ya Leverkusen mpaka mwaka 2027.Granit Xaka ambaye amewahi kua nahodha ndani ya timu hiyo kwa kipindi fulani atakumbukwa kwa mafanikio ambayo amekua ndani ya timu hiyo, Kiungo huyo amefanikiwa kushinda taji la kombe la Fa na timu hiyo pamoja na ngao ya jamii lakini vilevile alifanikiwa kufika fainali ya kombe la Europa na timu hiyo mwaka 2019.

Acha ujumbe