Kocha wa klabu ya Manchster City Pep Guardiola akizungumza na wanahabari amesema hajui kwanini klabu ya Real Madrid wanakua bora sana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.
Pep Guardiola wakati anaongea na wanahabari aliulizwa kwanini anafikiri Real Madrid wanakua bora sana kwenye ligi ya mabingwa ulaya zaidi kocha huyo alisema hajui ni kwanini kwasababu angekua anajua basi angeweza kuwafunga wakati amekutana nao.
Klabu ya Manchester City kesho itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Real Madrid kesho mchezo utakaopigwa katika dimba la Etihad ambapo ni uwanjani wa nyumbani wa Manchester City, Ikiwa ni mchezo wa marudiano ambapo mchezo wa awali ulimazika kwa sare ya bao moja kwa moja katika dimba la Bernabeu wiki iliyopita.
Guardiola wakati anaongea na wanahabari pia alisema kua anatambua ubora wa klabu ya Real Madrid na anatambua uimara wa kikosi chao, Lakini kitu cha muhimu ambacho kikosi chake kitakwenda kufanya siku ya kesho ni kuonesha ubora wao na wapi hatari yao inaweza kuwepo.
Kocha Guardiola vilevile amethibitisha kua beki wake Nathan Ake hatakuepo katika mchezo wa kesho, Hivo beki Akanji ataendelea kutumika katika upande wa kushoto ambao alikua anatumika raia huyo wa kimataifa wa Uholanzi ambaye bado anaendelea kusumbuliwa na majeraha.

