Beki wa kimataifa wa Italia na klabu ya Juventus Leonardo Bonucci amesema anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu ujao ikiwa mkataba wake ndani ya klabu hiyo utatamatika pia mwishoni mwa msimu ujao.
Beki Bonucci ambaye amekua kwenye klabu ya Juventus kwa muda mrefu akiitumikia timu hiyo na kushinda mataji tofauti tofauti, Lakini ametangaza baada ya msimu ujao kumalizika atatundika daluga akiwa na umri wa miaka 37 kwani mpaka sasa ana umri wa miaka 36.
Beki huyo wa kimataifa wa Italia wakati anaongea Mtandao wa You Tube wa klabu yake ya Juventus alisema pia wakati anakwenda kustaafu mwakani itakua ndio mwisho wa zama za uzuiaji kwa staili ya kiitaliano kama ambavyo walikua wakifanya wao na waliopita huko nyuma.
Bonucci ambaye ameitumikia Juventus michezo 500 mpaka sasa ameibua maswali kutokana na kauli yake hiyo ya kusema akistaafu yeye ndio utakua mwisho wa uzuiaji wa aina ya kiitaliano, Hii imeonesha kua beki huyo haoni beki mwingine wa Kiitaliano ambae atafata nyendo zao.
Beki Leanardo Bonucci atakumbukwa kwa mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya klabu ya Juventus kama kushinda mataji kadhaa ya Serie A, Copa Italia, Vilevile kucheza fainali mbili za ligi ya mabingwa ulaya na klabu hiyo, Lakini pia beki huyo amefanikiwa kwenye ngazi ya timu ya taifa kwani alifanikiwa kutwaa taji la Euro mwaka 2021 na timu ya taifa ya Italia.

