Ivan Toney Nje Miezi Nane Kwa Kosa la Kubashiri

Mshambuliaji wa klabu ya Brentford na timu ya taifa ya Uingereza Ivan Toney amefungiwa kujihusisha na shughuli zozote kimichezo kwa muda wa miezi nane na shirikisho la soka la Uingereza Fa baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na michezo ya ubashiri.

Ivan Toney alikua anatuhumiwa na kujihusisha na vitendo vya ubashiri ambavyo haviruhisiwi michezoni miezi kadhaa nyuma na uchunguzi ukawa unaendelea juu ya tuhuma hizo, Hivo leo ni wazi mchezaji huyo amekutwa na hatia na amehukumiwa miezi nane kutojihusisha na shughuli zozote za kimichezo.ivan toneyMchezaji huyo ambaye anafanya vizuri na klabu ya Brentford akiwa moja ya wafungaji bora kwenye ligi kuu ya Uingereza, Shirikisho la pira nchini humo kupitia taarifa yake limethibitisha kua mshambuliaji atakua nje ya uwanja kwa miezi nane na faini juu.

Ivan Toney anatarajiwa kurejea uwanjani Mwezi Januari mwaka 2024 ndipo ataweza kuanza kuitumikia timu yake ya Brentford kutokana na kutumikia adhabu ambayo amepewa baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na michezo ya kubashiri jambo ambalo halirusiwi na shirikisho.ivan toneyMshambuliaji Ivan Toney alikua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Brentford na kuhusishwa kutimkia timu kubwa, Lakini kutokana na sakata hili inaweza kumzibia nafasi ya kuweza kuondoka kwenye timu hiyo na kwenda kwenye klabu kubwa kwani ni ngumu klabu kulipia ada kubwa ya usajili kwa mchezaji ambaye atakua nje kwa nusu msimu.

Acha ujumbe