Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika kibabe baada ya kuifumua klabu ya Marumo Gallants kwa mabao mawili kwa moja katika uwanja wake wa nyumbani.
Yanga wamefanikiwa kutinga fainali ya Afrika ikiwa ni mara yao ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo baada ya kupata ushindi kwenye mikondo yote miwili ya hatua ya nusu fainali, Wananchi walifanikiwa kushinda kwa mabao mawili kwa bila mchezo uliomalizika na kufanikiwa kurudia walichokifanya wiki iliyopita.
Kocha Nassrdine Nabi alikwenda na mkakati uleule ambao ulimpatia matokeo katika dimba la Benjamin Mkapa Jumatano iliyopita, Kuwaruhusu Marumo kukaa na mpira halafu wao wanatumia mipira ya kushtukiza na karata hiyo imefanikiwa tena leo nchini Afrika Kusini.
Mabao ya Fiston Kalala Mayele kipindi cha kwanza na Kenedy Musonda yameiwezesha Yanga kutinga fainali kibabe kwa jumla ya mabao manne kwa moja, Huku Fiston Kalala Mayele akiwa nyota wa mchezo kwani amekua na kiwango bora sana baada ya kufunga baoa moja na kupiga pasi ya bao kwenda kwa Kenedy Musonda.

