Kocha wa klabu ya Manchester City raia wa kimataifa wa Hispania Pep Guardiola amesema kushinda taji la ulaya ni ngumu zaidi kuliko michuano mingine.
Guardiola aliyasema hayo wakati anazungumza na wachambuzi jana baada ya mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kati ya klabu yake ya Manchester City dhidi ya Inter Milan ambapo walishinda bao moja kwa bila na kutwaa taji hilo.
Kocha huyo ameweka wazi alihitaji kubadilika zaidi katika safu ya ulinzi na kuzuia zaidi kwenye boksi lao kitu ambacho anaeleza walikikosa katika misimu kadhaa iliyopita na kupelekea kukosa taji hilo mwaka 2021 mbele ya klabu ya Chelsea lakini ameeleza msimu huu wamebadilika zaidi kwenye kuzuia na kushinda taji.
Kocha Guardiola amekua akinyooeshewa vidole mara kwa mara licha ya kucheza mpira mzuri wakuvutia ndani ya Man City na kutwaa mataji kadhaa, Lakini akifeli kutwaa taji la ulaya na watu wengi wakidai alikosa nidhamu ya ulinzi kitu ambacho ameonesha kukiri na kukifanyia kazi msimu hatimae kutwaa taji la ulaya.
Guardiola sasa anakua kocha pekee kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja mara mbili kwani ameshawahi kufanya hivyo akiwa na klabu ya Barcelona mwaka 2009 na jana akifanikiwa kurudia na klabu ya Manchester City.

