Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe akanusha suala lake la kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo na kujiunga na wababe wa soka nchini Hispania klabu ya Real Madrid.
Mbappe ametoka hadharani kukanusha taarifa za yeye kukataa kuongeza mkataba wake ndani ya klabu ya PSG mpaka mwaka 2025, Huku akidai dhamira yake bado ni ileile kusalia ndani ya klabu ya PSG kwasababu ana furaha kuwepo klabuni hapo.
Mfungaji bora huyo wa ligi kuu ya Ufaransa amekanusha habari hizo baada ya kusambaa kwa taarifa kua hataongeza mkataba ndani ya timu hiyo na anatarajia kuondoka bure ndani ya timu hiyo, Huku ikitaarifiwa klabu hiyo haiko tayari kumuachia aondoke bure.
Kylian Mbappe amekua hana msimamo mara kwa mara juu ya hatma yake ndani ya klabu ya PSG kwani alieleza kua ana furaha ndani ya klabu ya hiyo, Lakini taarifa za nyuma ya pazia zinaeleza kua ana ndoto ya kucheza klabu ya Real Madrid bado.
Klabu ya Real Madrid nayo bado inamuhesabu Mbappe katika mipango yake kupitia kwa Florentino Perez rais wa klabu ya Real Madrid, Huku wakiwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo dirisha lijalo kwa uhamisho huru na PSG wakiwa hawako tayari kumuachia bure hivo watahitaji kumuachia dirisha hili.

